Thursday, 6 April 2017

DONDOO ZA UPANDAJI MAZAO

MAMBO MANNE YA KUZINGATIA KABLA YA  KUPANDA MAZAO

Kwa mkulima anayechukulia kilimo kama biashara, ni muhimu ajiulize je, ni wakati gani sahihi
wa kupanda? Kwa wakulima wengi jawabu linalokuja kwa fikra zetu mara moja ni
wakati wa mvua. La hasha!.Wakati mzuri wa kupanda unatambulika vyema
tunapozingatia mambo fulani katika soko kama vile:
•  Ni wakati au muda gani mmea wako utakomaa?
•  Wakati ambao uhitaji (demand) wa zao unakuwa juu.
•  Wakati ambapo bei ya mazao ni nzuri kwa mkulima.
•  Wakati ambapo utoaji (supply) wa zao uko chini kabisa.

Ni muhimu kwa mkulima kuwa na mwongozo wa upandaji akizingatia uhitaji na ugavi
wa mazao sokoni.

No comments:

Post a Comment